Hatimaye Miss Tanzania 2014 , Sitti Abbas Mtemvu ajivua taji
Sitti
Abas Mtemvu amelivua taji hilo baada ya kuiandikia barua Kamati ya Miss
Tanzania, November 5 mwaka huu, kuhusiana na uamuzi wake huo.
Mrembo
huyo alikuwa akikabiliwa na shutuma za kudanganya umri wake, jambo
ambalo lilililazimu Baraza la Sanaa la Taifa, (Basata) kutokana na agizo
la wizara husika kufuatilia ukweli wake.
“Baada
ya kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania kumezuka shutuma mbalimbali
dhidi yangu. Wameniwekea maneno mengi sana mdomoni kwamba nimesema
wakati siyo,” amesema kwenye barua hiyo.
“Shutuma
hizo zimeandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari, blogs na mitandao
ya kijamii, kiasi ambacho naweza hata kuhatarisha maisha yangu. Sasa
kwa hiari yangu tena bila kushawishiwa na mtu na kwa kulinda heshima
yangu na familia yangu natamka rasmi kuvua taji la urembo la Miss
Tanzania 2014,” ameongeza.
“Napenda
niwashukuru wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo
nilipoingia katika mashindano haya katika ngazi ya taifa, na warembo
wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja na wote tuliokuwa nao katika fainali
za Taifa. Pia napenda kutuma shukrani za dhati kwa waandaji wote wa
kituo cha Chang’ombe, Temeke na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania kwa
mafunzo mbalimbali niliyopata. Nawashukuru pia waandishi wote kwa
mchango wenu, pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na Baraza
la Sanaa kwa busara zenu.”
“Leo
nalivuta taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi
Mungu bado ninalo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi huo
niliochukua.”
Nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa mshindi wa pili, Lilian Kamanzima.
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga (kushoto) akionyesha barua ya Miss Tanzania, Sitti Abas Mtemvu baada ya kujivua taji hilo.
Waandishi wa habari wakiendelea kufanya yao.
Miss Tanzania aliyechukua nafasi ya Sitti Mtemvu, Lilian Kamanzima akiongea na wanahabari (hawapo pichani)
Lilian Kamanzima katika pozi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga (kushoto) akionyesha barua ya Miss Tanzania, Sitti Abas Mtemvu baada ya kujivua taji hilo.
Waandishi wa habari wakiendelea kufanya yao.
Miss Tanzania aliyechukua nafasi ya Sitti Mtemvu, Lilian Kamanzima akiongea na wanahabari (hawapo pichani)
Lilian Kamanzima katika pozi.
0 comments:
Post a Comment