Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua


Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua
Watoto wadogo hasa wale ambao bado wananyonya na ndio kwanza wamenzishwa vyakula vinginevyo zaidi ya maziwa, mara nyingi hupatwa na choo kigumu au kukosa choo kabisa hali tunayoiita kimombo, constipation. Hali hiyo huanza pale mtoto anapoachishwa maziwa ya mama na kuanza kunyweshwa maziwa ya kopo au mengineyo au pia anapoanzishwa kula vyakula vingine zaidi ya maziwa. Mara nyingi watoto wanaonyonya maziwa ya mama huwa hawasumbuliwa na tatizo hilo, bali tatizo hilo huanza kujitokeza pale wanapoanza kulishwa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama. Pia mama ambaye tayari mwenyewe anasumbuliwa na tatizo la kukosa choo, huenda mwanae pia akasumbuliwa na tatizo hilo.
Mtoto mwenye tatizo la kukosa choo huwa anapata choo wa shida huku akisumbuliwa na tumbo na kupata choo kigumu. Wakati mwingine hulia wakati akipata choo huku akijiminya na kukunja uso. Muone daktari iwapo mtoto ana umri wa chini ya mwezi mmoja na hajapata choo kwa siku 4.
Iwapo mtoto wako mchanga au mdogo ana tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu kwanza wasiliana na daktari au mpeleke hospitalini ili upate ushari wa daktari. Pia unashauriwa kujaribu njia zifuatazo:
1. Jaribu kumpa mtoto wako maji safi na salama kuanzia mililita 60 hadi 120 kwa siku. Punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa. Ni bora maji ya mtoto yachemshwe na kufunikwa vyema.
2. Iwapo maji hayasaidii, jaribu pia kumpa juisi za matunda. Mpe mtoto wako juisi ya tufaha (apple), pea au prune iliyotengenezwa kwa kutumia maji salama na safi kila siku. Anza kwa mililita 60 hadi 120 kwa siku na punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa.
3. Jitahidi kumpa mwanao chakula chenye ufumwele au fiber. Iwapo mwanao ameanza kula vyakula vigumu, basi mpe vyakula vyenye ufumwele kuliko vyakula vyenye wanga, kama vile tumia unga wa shayiri au tunda la apple na pea lililopondwa pondwa vyema na kuwa kama uji. Epuka kumpa mtoto cereal ya mchele au uji wa mchele kama anatatizo la kukosa choo au kufunga choo.
4. Jiepushe kumpa mtoto wako vyakula vyenye wanga na sukari na vyakula vinavyotengenezwa kwa unga uliokobolewa.
5. Mpake mwanao mafuta kidogo sehemu inayotoka choo kikubwa ili kurahisisha utokaji wa kinyesi. Usitumia mafuta ya madini (mineral oil) au dawa za kulainisha choo na za kuharishwa katika kutibu tatizo hilo la kukosa choo la mtoto.
6. Kukosa choo watoto wadogo mara chache huwa kunasababishwa na magonjwa kama vile Hirschsprung ugonjwa wa kumee neva katika utumbo, au Cystic Fibrosis. Muone daktari au mpeleke mtoto wako hospitalini kama tatizo hilo la kukosa choo linaendelea hata baada ya kubadilisha aina ya chakula cha mtoto au linaambatana na dalili nyingine kama vile kutapika au mtoto kukosa utulivu na kuhangaika.
7. Kuna baadhi ya watoto wanakosa choo au kuwa na choo kigumu kutokana na kutumia maziwa ya ng’ombe. Iwapo umetumia dawa na umefuata maelekezo ya kuondoa ukosefu wa choo na hukufanikiwa. Katisha kumpa mtoto maziwa ya ng’ombe kwa siku mbili au tatu, baada ya siku hizo iwapo bado hajaacha choo badi endelea kumpa maziwa hayo, na pengine tatizo hilo halisababishwi na maziwa ya ng’ombe.
8. Mwogeshe au mweke mwanao katika beseni la maji ya uvuguvugu na hakikisha maji yanafika hadi kifuani. Mkande mtoto tumbo lake wakati akiwa majini na njia hiyo husaidia kulegeza misuli ya mwili wa mtoto, na kumsaidia kupata chook wa urahisi.
N.B Ukosefu wa choo kwa watu wazima baadhi ya wakati huandamana na magonjwa kama vile Arthritis, Appendicitis, Cataract, saratani, shinikizo la damu, Rheumatism na kadhalika lakini kwa watoto huenda tatizo hilo likawa halisababishwi na maradhi hayo.
Utafiti unaonyesha kuwa hakuna uhusiano wowote kuhusu kukosa choo mtoto na kupewa nyongeza ya chuma au Iron Supplement. Hivyo usimkatishe kumpa mwanao chuma iwapo anakosa choo. Kwani chum ni muhimu sana katika kuzuia upungufu wa damu mwilini kwa mtoto wako mdogo.

6 comments:

Paul Akwilini said...
Nashukuru kwa maelezo yako mazuri ngoja nijaribu kulifuata kwani mwanao anasumbuliwa na hilo tatizo. Pia ni kweli mama yake alikuwa anapata shida ya choo tangu akiwa na mimba hadi hivi sasa anapata nae choo kigumu na humchukua siku hadi kupata. Asante sana!
The great said...
Ahsante kwa somo nzuri amnalo halina gharama nyingi,mungu awabariki
Anonymous said...
Nashukuru sana kwa somo hili zuri maana hata mimi nina mtoto wa miezi 5 ila huwa hasumbuliwi sana na hili tatizo.

Lakini naomba kuuliza kuna watu walinambia kuwa mtoto anapopata choo kigumu au kupitisha siku zaidi ya mbili naweza kumpa CASTOR OIL...je ni sahihi au yana madhara?

Mdau...Musoma
Anonymous said...
Nilikua sijaiona hii blog mpaka leo ndio nilikua nasoma soma mara nikaikumba. Ni blog nzuri na nimependa unavyoelezea vitu.

Ninachoomba baada ya kusoma post kadhaa ni heri uweke warning hapo juu wasomaji wasome waelewe kuwa hapa ni unashauri kutokana na articles au ujuzi ila wasichukue ushauri wako kama final answer. Hiyo ndio inatakiwa kwa site zote zinazoelezea mambo ya afya. Unajua kwetu wengine kumwona Dr mpaka tuwe taabani tunapenda kuambiana tu. Utasikia mtu anasema nasikia kizunguzungu mtu mwingine anasema aah hiyo umechoka tu, huna maji mwilini kumbe una jambo kubwa zaidi.Before you know mtu androp dead. Na technologia za sasa hivi wengi wataingia tu kwenye PC na kuangalia unachoandika na kufikiria kama ndio solution. Hiyo disclaimer itasaidia kuwakumbusha watu na kuokoa maisha ya wengi..

2nd unaposema umpe mtoto maji hujaelezea ni mtoto wa umri gani. Unajua kwetu tunafanya vitu vingi bila scientific research ni ile kutokana na bibi alifanya basi na mama kafanya hivyo na mimi nitafanya. Ndio kuna vitu vingine haviitaji research alakini kuna vingine ukiangalia au kulinganisha utajua kuwa kweli ni Mungu anayetulinda au kunaambao watoto wanakufa kumbe mtu ungeelewa na kufanya vinavyotakiwa ungesaidia kuponyesha maisha ya watoto. Kwa vile mimi nilijifungua mbali, mama alikuja mwanangu alikua na miezi 7 hivyo uzazi wote nilifanya bila ya kuwa na mama yangu au hata watanzania wenzangu karibu ilibidi nitegemee madoctor, nurses na consultants tu kwa hiyo nilijifunza vitu vingi sana. Mtoto chini ya miezi sita hairuhusiwi kumpa maji. Nakumbuka nilikua naongea na mama namwambia mtoto analia mama ansema mpe maji. Sina notes zangu sasa hivi lakini nitazitafuta nikuandikieuwaonyeshe watu kuna madhara sana.

Mtoto akifungwa choo kuna Karo syrup inafanya kazi sana. Nadhani hata tanzania ipo na pia kama unavyonyesha ujue kuwa mama mwenye mtoto hana maji mwilini ndio maana mtoto hayapati maji. Ukiwa unanyonyesha baada ya kunywa soup tunazotengenezewa unatakiwa unywe maji sana. Nilikua nakunywa maji gallon moja kwa siku. Ikamaliza kabisa matatizo ya choo.

Kama mtoto anayekula chakula ndio hivyo vyakula vyenye fiber na mboga za majani zitasaidia

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger