Saratani ni mojawapo ya magonjwa hatari ambayo yanaua watu wengi kote duniani na tiba yake ni ngumu sana.
Wachache sana wanaopata ugonjwa huu hufa. Wale wanaowahi matibabu ugonjwa unapokuwa katika hatua za mwanzo walio wengi hupona na kuokoa maisha yao. Makala hii inaelezea nini kinasababisha na namna ya kuepukana na ugonjwa wa saratani
Saratani hutokana na seli za mwili zilizopoteza mfumo wake wa kugawanyika na kutokuwa katika mfumo wake wa kawaida.Seli hizi hukua bila kufuata utaratibu maalumu na hivyo kusababisha uvimbe mwilini.
Seli hizo za saratani huweza kusambaa mwilini kwa nyia ya damu au limfu( kwa kiiengereza (lymph). Saratani hutokea sehemu mbalimbali mwilini kama kwenye matiti,koo,kinywa,shingo ya kizazi ya kina mama,ovari,tezi dume na katika ngozi.
Makundi Mawili ya Saratani
Saratani imegawanyika katika makundi wawili kutokana na sababu zake1. Ya kurithi kutokana na ukoo
2. Ya kimazingira
Sababu kubwa zinazosababisha saratani ni zile za kimazingira kuliko urithi wa vinasaba.
Vitu Vinavyosababisha Saratani
Sababu kuu za saratani ni mtindo wa maisha usiofaa ambao uatafsiriwa kwa mambo yafuatayo:– Ulaji mbaya na unene
Ulaji wa vyakula vyenye nishati lishe kwa wingi(mafuta,sukari na wanga) ambavyo husababisha unene usiofaa.
Unene wa mwili unaongeza hatari ya kupata saratani hasa ya figo,uzazi,matiti,utumbo mpana na kibofu.
– Ulaji wa nyama nyekundu
Nyama nyekundu na hasa zile zilizosindikwa zinahusishwa na kusababisha saratani ya kinwaya,utumbo mpana na tezi dume.
Vyakula vinavyosindikwa kama soseji na bakoni uwekwa kemikali ziitwazo nitrosamines ambazo husababisha saratani.
– Unywaji Pombe kwa Wingi
Unywaji wa pombe unaweza kusababisha upatikanaji wa saratani ya koo ,tumbo na tezi dume.
Pombe kama bia ambzo zina kemikali aina ya nitrosamine ambayo husababisha saratani.
– Vyakula vyemye Ukungu
Vyakula vilivoota ukungu kama karanga,mkate,samaki waliozeshwa kama sangara wa kubanika,na samaki wa baharini ambao huvundikwa hutengeneza kemikali iitwayo aflatoxins ambayo husababbisha saratani ya ini.
– Sigara
Uvutaji sigara na bidhaa zinazotokana na tumbaku husababisha saratani ya koo,kinywa na mapafu.
– Kutofanya Mazoezi au Kazi Nzito
Maisha ya kisasa hasa mijini ambako watu hupanda magari na kuanya kazi za maofisini ambazo hazisababishi mwili kujishughulisha wapo katika hatari kubwa ya kupata saratani ya utumbo mpana,tumbo,matiti,mapafu na tezi dume.
– Mionzi Hatarishi
Mionzi au dawa za viwandani nazo pia zinaweza kukusababishia saratani.
– Madini Hatarishi
Madini kama risasi, zebaki , uraniamu na asbestos yanaweza kusababisha saratani yakiingia kwa wingi mwilini.
Zebaki inapatikana sana katika vyakula hasa vya baharini na ziwani na katika vipodozi na dawa za binadamu.
-Virusi
Virusi kama hepatitis B husababisha saratani ya ini vingine ni HPV- himan papiloma ambavyo husababisha saratani ya shingo la kizazi.
Mambo ya Kufanya Kuepukana na Ugonjwa wa Saratani
Tafiti nyingi zilizolizofanywa zinaonesha kuwa sababu kuu
zinazosababisha saratani ni mtindo wa maisha usiofaa kama ulaji usiofaa
na kutofanya mazoezi ua mwiliIli kuepukana na ugonjwa wa saratani au kupunguza uwezekano wa kupata saratani ni muhimu kuzingatia yafuatayo:
1. Kula zaidi vyakula vya mimea na nafaka zisizokobolewa
Matokeo ya tafiti yanaonesha kuwa vyakula hivi vinapunguza uwezekano wa kupata saratani
Hakikisha unakula mboga mboga za kijani na rangi nyingine kama njano,zambarau n.k
Kula nafaka zisizokobolewa kama unga wa dona,mchele wa brauni,unga wa ngano usiokobolewa,mtama na ulezi.
2. Kuwa na Uzito Uliosahihi
Uzito mkubwa uliopitiliza ni hatari na husababisha saratani. Hakikisha uwiano wa urefu na uzito wako (BMI- Body -to-Mass Index) ni sahihi ambayo ni 18 -25 kwa mtu mzima na mwenye afya nzuri unashauriwa kuwa na uwiano wa 21-23.
Punguza vyakula vinavyonenepesha mwili kama vyenye mafuta na sukari kwa wingi. Vyakula vyenye mafuta kwa wingi kama chipsi na vitumbua mfano ni hatari kwa afya yako.
Vyakula vyenye sukari ni kama soda,chokoleti,keki,barafu na iskrimu na juisi bandia.
3. Fanya mazoezi ya mwili
Fanya mazozi ya mwili kila siku. Dakika 15-30 tu zinatosha kufanya mazoezi kwa afya njema.
Ukikosa muda fanya anagalau mara 3 kwa wiki kwa muda usiopungua dakika 30.
Kukimbia(jogging) ni njia rahisi ya kufanya mazoezi yanayohusisha mwili mzima. Ukiweza jiunge katika timu ya mpira au klabu za mazoezi ya ndani.
Tembea kwa miguu pale inapobidi. Rafiki yangu mmoja ambaye ana gari ameweka ratiba ya kutotumia gari wakati wa mwisho wa juma. Anapanda dalala na kutembea kwa sehemu kubwa. Unaweza ukafanya pia.
4. Punguza au Acha kula Nyama Nyekundu
Ukiachia saratani nyama nyekundu imetambulika kusababisha madhara mengi na makubwa kwa binadamu.
Amua sasa kuachana nayo. Hamia katika samaki na kuku kwa kuanzia na baadae huenda ukaachana na hizo nyingine pia.
Nyama ya nguruwe maarufu kam Kitimoto ni nyama nyekundu na ni hatari kwa afya yako . Heri wale ambao hata dini zao zilikataza nyama hii ya Nguruwe kwani wameepuka hatari.
5. Epukana na Nyama za kusindikwa.
Nyama za makopo na soseji zinasababisha saratani kutokana na kemikali za kutunzia zisioze na pia huwekwa chumvi nyingi sana ambayo ni hatari kwa afya.
6. Punguza Matumizi ya Chumvi
Chumvi ya kupita kiasi inaongeza uwezekano wa kupata saratani hivyo ni hatari. Tumia chumvi kwa kiasi kidogo kwa afya njema. Binadamu anahitaji gramu 5 tu kwa siku sawa na kijoko kidogo cha chai.
Usiongeze chumvi wakati wa kula,chumvi isiyoyeyuka nia hatari zaidi.
7. Acha kula Vyakula vyenye Ukungu
Acha kula nafaka na kundekunde zilizootesha ukungu hasa kwa kutohifadhiwa vyema. Vyakula hivi vinatoa sumu ya aflatoxin
8. Usivute Sigara
Uvutaji wa sigara ni hatari na huenda ukakusababishia saratani ya koo,kinywa na mapafu. Acha kuvuta sigara ili kuepukana na ugonjwa wa saratani. Fikiria kidogo,kwanini ufe kwa sababu ya moshi tu?.
9. Punguza au Acha Pombe Kabisa
Ukiacha pombe utapunguza uwezekano wa kupata saratani na hivyo kuwa salama zaidi.
Achana na pombe, kuna madhara mengi sana ya kunywa pombe ukiachia ya saratani.
Badilisha Mtindo wa Maisha na Uwe Salama na Saratani
Namna ya kuishi kunachangia kwa kiasi kikubwa kupata saratani au la. Chagua mtindo ulio bora na salama kama ilivyoshauriwa katika mada hii juu ya kuepukana na ugonjwa wa saratani.Afya yako ni jukumu lako mwenyewe na kupanga ni kuchagua. Panga kuishi mtindo wa maisha ulio bora na salama chagua kuishi bila saratani.
Kama umeona mada hii kuwa na manufaa kwako,basi washirikishe wengine nao wafaidike. Bonyeza vitufe hapa chini kushirikisha marafiki katika mitandao ya kijamii.
Kama una hoja ua maswali tafadhali andika katika kisanduku chini ya mada hii.
Nawatakieni afya njema, saratani inaepukika.[:]
0 comments:
Post a Comment