Namna ya Kuhakiki na Kuchagua Kampuni ya Biashara ya Mtandao ya Kujiunga
Ili kufanikiwa katika biashara ya mtandao ni muhimu sana kufahamu namna ya kuhakiki na kuchagua kampuni sahihi ya kujiunga na kufanya nayo kazi. Takwimu zinasema kuwa takribani 90% ya wasambazaji wa biashara ya mtandao wanafeli. Mojawapo ya sababu kubwa ni kuchagua kampuni isiyo sahihi zikiwemo sababu nyingine pia nyingi elimu ya biashara ikiwa kama sababu nyingine kubwa ya watu kushindwa katika biashara hii.
Kampuni sahihi ni ipi?
Ni ile ambayo ina bidhaa bora na yenye manufaa,rahisi kuiuza na kumshirikisha mwingine. Ni kampuni yenye uongozi bora na yenye kutoa malipo mazuri kwa wasambazaji wake na kuwawezesha kuboresha maisha yao kutokana na juhudi zao.Mambo 4 ya Kuangalia Kuchagua Kampuni Sahihi ya Biashara ya Mtandao
Kuna mambo yapatayo matatu makuu ya kuangalia ili kuchagua kampuni sahihi litakalokupa nafasi kubwa ya kufanikiwa.-
Umri wa Kampuni
Biashara yenye miaka 10 na kuendelea ni thabiti zaidi na ni komavu.
Baadhi ya makampuni yaliyopo Tanzania na umri wake ni:
- GNLD : Miaka 58 (Toka 1958)
- Forever Living Products: 38 (toka 1978)
- Trevo: Miaka 6 (Toka 2010)
- Rifaro: Miaka 5 (Toka 2011)
- Oriflame: Miaka 49 (Toka 1967)
-
Bidhaa au Huduma Inayotolewa
Ukitaka kujiunga na kampuni yoyote ya mtandao hakikisha unaifahamu bidhaa inayouza na sifa zake zote. Bidhaa yenye kutoa faida kwa watu na yenye uhitaji. Itakuwia vigumu kumshari mtu yeyote unayempenda na kumjali kutumia bidhaa isiyo na manufaa kwake. Kama bidhaa hiyo huwezi kuiuza kwa mama au baba yako, basi hiyo kampuni si sahihi. Na kama ni kinyume chake basi ikimbilie na jiunge mara moja.
-
Mpango wa Malipo
Ifahamike kuwa dhumuni kuu la yeyote kujiunga na katika biashara ya mtandao ni kupata huduma au bidhaa (matumizi) na kupata kipato cha fedha na hata kujenga utajiri. Sehemu ya pili ya kuongeza kipato inategemea pia mpango wa malipo unaotumika ukiachia bidhaa na uzuri wake.
Angalau mfumo ambao unakuwezesha kukuza timu kwa haraka na kufaidika na timu unayoijenga.
Makampuni mengine yanaweka kikomo cha watu wa kuwaingiza moja kwa moja katika kizazi cha kwanza au kikomo cha vizazi chini yako.
Kampuni lisilikupa kikomo cha watu wa kuwaingiza binafsi ni bora zaidi na linakupa nafasi kubwa ya kufanikiwa kuliko lebye kukupa kikomo.
Kampuni lisilo na kikomo cha idadi ya vizazi chini yako au lenye kuruhusu vizazi vingi zaidi ni nzuri zaidi.
Pia viwango vya malipo vinavyotolewa kwa kuingiza wanachama wapya na kwa manunuzi yako binafsi na manunuzi ya vizazi vyako. Kampuni lenye kutoa viwango vikubwa litakufaa zaidi na kinakupa nafasi ya kufanikiwa kwa haraka sana.
Angalia baadhi ya mipango ya makampuni makubwa Tanzania:
- GNLD
- FLP
- TREVO
- RIFARO
- ORIFLAME
-
Malipo kwa Wasambazaji
Makampuni mengine yanalipa kwa mwezi na mengine yanalipa kila wiki au vyote kwa wiki na kwa mwezi.
Hakikisha kampuni unalojiunga linalipa na linalipa kwa wakayi na kwa namna iliyo rahisi kupata fedha zako.
Uluzia wale waliokwisha jiunga kama wanalipwa inavyostahili.
Uchaguzi:
Baada ya kuangalia mambo hayo manne makuu kwa kampuni husika na kujiridhisha kuwa yamekidhi vigezo basi unaweza kujiunga na hakuna sababu ya kuogopa. Watu wengi wenye kuangalia biashara ya mtandao wamekuwa na hofu kubwa kujiunga. Unatakiwa kuwa na elimu juu ya biashara yoyote duniani kabla hujaifanya na vivyo hivyo kwa biashara ya mtandao.Kuna fursa kubwa ya mafanikio ya kipato katika biashara ya mtandao. Unatumia nguvu ya umoja katika kufanikiwa badala ya nguvu zako wewe binafsi pekee.
Bila shaka mkala hii itakuwa ya msaada katika kufanya maamuzi ya kampuni ipi itakufaa kujiunga na inayokupa fursa ya mafanikio kifedha pia ukiachia mbali faida unayopata kwa kutumia bidhaa au huduma.
0 comments:
Post a Comment