Maneno Mabaya 10 ya Kutosema Kwa Mwenza Wako
Mojawapo ya nguzo kuu kabisa ya mahusiano mazuri ni mawasiliano. Mawasiliano mazuri yanahusisha vitu viwili vikubwa, kuwa na ujumbe wa kusema na namna ya kusema ujumbe wako.
Maneno ni kitu hatari sana katika mahusiano yakitumiwa vibaya na yakitumika vizuri ni nguzo kubwa ya mahusiano mazuri na yenye furaha.
Hivyo unatakiwa kupangilia maneno yako unapoongea na mwenza wako ili kupata athari chanya. Ifahamike kuwa maneno mabaya yakisha semwa hayarudi mdomoni na madhara yake yatabaki siku zote hata kama mwenza wako atasema kuwa amesamehe au kusahau.
Maneno yafuatayo ni hatari kwa kuwa yanaleta madhara makubwa moyoni mwa mlengwa na ni vyema kuzuia kuyatamka kwa namna yoyote ile.
Maneno 10 Mabaya Ambayo Hutakiwi Kusema Kwa Mwenza Wako:
-
Maneno ya Matusi
Useseme maneno mabaya yanayomshusha mweza wako mfano kuhusu mwonekano mbaya wa mwenza wako kama “sura mbaya”,”Mnene kama nguruwe” n.k
-
“Nakuchukia”
-
“Ameiga Tabia Zako”
-
Kumfananisha Tabia Mbaya za Mwenza na Wazazi Wake
-
“Acha!Nitafanya Mwenyewe”
-
Maneno Mabaya ya Kukatisha Tamaa
Ni muhimu kwa wenza kupeana moyo na kusaidiana ili wote muende mbele kwa pamoja. Umoja ni nguvu.
-
“Mtoto wangu”
-
“Haya yote ni makosa yako”
-
Kutolea Mifano Mahusiano ya Zamani
-
Maneno juu ya Kuachana
Mfano “Kwa mtindo huu mimi nafikiri hatutafika mbali”
Mwenza wako ataanza kujiandaa kuachana na hatajiachia kwa asilimia zote kwa mapenzi na mipango ya pamoja. Maneno haya yanajenga utengano taratibu ndani ya moyo wako na wa mwenza wako.
Mwisho
Kama nilivyosema mwanzoni,mawasiliano ni nguzo ya mahusiano mazuri kati ya weza wawili. Ni kitu ambacho kila mmoja anatakiwa kujifunza na kukitilia maanani hasa kwa kujua mahusiano ya mke na mume yana changamoto kubwa kutokana na utofauti wa kihisia na kitafakuri kati ya mke na mume.Mwanamke na mwanaume wanaonekana kama viumbe tofauti toka sayari tofauti kutokana na namna zao tofauti za kuwasiliana na kuelewa ujumbe toka kwa mwingine.
Busara za kuchambua nini cha kusema na kipi kuacha kutasaidia sana kuboresha mahusiano na mwenza wako
Nini changamoto zako na mwenza wako katika mawasiliano? Maneno mabaya yapi ambayo yanakukera kuambiwa na mweza wako na unafikiri si vyema kuyatumika kwa weza ukiacha haya? Tafadhari shiriki kujadili kwa kuandika katika kisanduku hapa chini.
Asante na nawatakia mahusiano na mwasiliano mema
0 comments:
Post a Comment