1.
Jiandae kiakili kwanza kuwa sasa umefika wakati wa wewe kuingia kwenye
ndoa, sio unakurupuka tu ukahisi ndoa nayo huvamiwa vamiwa tu, utakula
za uso halafu ujutie hiyo ndoa.
2. Ingia katika ndoa na mtu
umpendaye kwa dhati haijalishi ni maskini au tajiri maana kama umempenda
mtu kwa moyo wote hata kama mkikutana na majaribu yapi mtasameheana na kusonga mbele
3. Jipange kimaisha japo kidogo maana unakuta mtu hana hata kitanda
wala godoro au chumba cha kuishi eti naye anataka kuoa, hata kama ni
kuvumiliana si kwa aina hiyo, hapo itakuwa kutesana baadala ya
kuvumiliana kwakweli. Japo hali ni mbaya jitahidi upange gheto zuri
halafu nunua japo godoro, sasa kama hilo nalo huwezi hata usioe maana
utaishi vipi sasa na huyo mkeo, si mtashindwa hata kula?
4.
Chagua mtu ambaye unaona unaendana naye kitabia na vitu anavyopenda
kufanya, wewe kama hupendi tabia ya mvuta sigara kamwe usikubali
kuolewa/kuoa mvuta sigara, kama hupendi mlevi kamwe usikubali
kuolewa/kuoa mlevi maana hicho kinachokukera na yeye anakipenda kitakuwa
chanzo cha matatizo kwenye ndoa yenu
5. Kuwa tayari kwa kila
kitu, kusalitiwa, kuibiwa mme/mke, kupigana, kuchekeana na kila kitu
maana haya yote yapo ndani ya ndoa, usijidanganye kuwa ndoa ni tambarale
tu kwahiyo iandae akili
yako kwa yote hayo
6. Jifunze kuwa
mtunzaji siri kabla hujaingia kwenye ndoa maana katika ndoa kuna vitu
vingi hujitokeza, sasa kama mke/mmeo wako hakuridhishi halafu unaenda
kutangaza nje ya ndoa ukiibiwa usije ukalaumu mtu.
Share na marafiki zako wajue , pia ongezea lingine unalolijua kwa kukomenti hapo chini.
MAMBO 6 YA KUFANYA KABLA HUJAAMUA KUINGIA KWENYE NDOA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment