FEDHA
zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kuwezesha wananchi kiuchumi
maarufu kama mabilioni ya Kikwete, imeelezwa sehemu hazikutumika huku
nyingine zilizokopwa hadi sasa hazijarejeshwa.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji na Uwezeshaji, Christopher Chiza
alitoa taarifa hiyo jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la
Mbunge wa Viti Maalumu, Maryam Salumu Msabaha (Chadema).
Mbunge
huyo alisema mikopo iliyotolewa kwa fedha hizo ambazo kwa upande wa
Zanzibar zilijulikana kama mabilioni ya Karume na kwa Tanzania Bara
mabilioni ya Kikwete, watu hawakurejesha.
Hivyo
alitaka kufahamu ni hatua gani serikali inachukua kwa watu hao. Chiza
alisema Zanzibar walipata Sh milioni 600 na serikali yao ikaongeza Sh m i
l i o n i 600 na kufanya jumla yote kuwa Sh b i l i o n i 1.2.
Hata h i v y o , a l i s e m a k w a pande zote, Zanzibar na Tanzania Bara, kulikuwa na changamoto zilizojitokeza. “Zipo fedha ambazo hazijatumika….Mkaguzi mkuu wa ndani amefanya ukaguzi wa fedha zote,”
alisema Chiza na kuongeza kuwa taarifa ya mkaguzi, itaeleza ni nani
alipata mkopo wa fedha hizo na ni nani hakurejesha kwa ajili ya kuchukua
hatua stahiki.
Awali
katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu, Faida Mohamed Bakari
(CCM) alitaka kufahamu ni wafanyabiashara wangapi wenye ulemavu
walipatiwa mikopo kupitia fedha hizo.
Waziri
Chiza alisema mpango huo wa kuwezesha wananchi kiuchumi, ulikuwa na
madhumuni ya kuwezesha wananchi kiuchumi na kuongeza ajira kwa wanawake
na vijana vijijini na mijini kwa kuwapatia mikopo bila kujali maumbile
yao.
Alisema
chini ya mpango huo, mikopo ilitolewa katika awamu mbili kupitia benki
na asasi za kifedha, zilizoteuliwa na serikali baada ya kukidhi vigezo
ambapo jumla ya Sh bilioni 43.69 zilitolewa na kunufaisha wajasiriamali
74,593.
Kwa
upande wa Tanzania Bara, wananchi waliohitaji mikopo hiyo walitakiwa
kujaza fomu ambazo hazikuwa na kipengele kinachoainisha iwapo mwombaji
ni mtu mwenye ulemavu au siyo.
Waziri
alisema kutokana na utaratibu huo, imekuwa vigumu kutoa takwimu za watu
wenye ulemavu waliopata mkopo, aina ya ulemavu walio nao na sehemu
wanakotoka pamoja na aina ya biashara wanazofanya kama alivyotaka
mbunge.
Hata
hivyo, alimshukuru Mbunge Faida na kusema serikali imepokea swali lake
kama changamoto ya kufanyia kazi, ambayo itachochea kubuni upya
utaratibu wa utoaji mikopo hiyo kwa kuzingatia vigezo vya ziada kwa watu
na makundi maalumu wakiwemo wenye ulemavu wa viungo.
0 comments:
Post a Comment