Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe amesema Watanzania
wamepoteza imani na Jeshi la Polisi na ameliagiza kujitathmini na kutoa
majibu kuhusu kukamatwa kwa vijana 1,200 wa kikundi cha uhalifu maarufu
Panya Road.
Waziri
Chikawe aliyekuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka kwa maofisa
waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini, amelitaka jeshi hilo kujiuliza na
kutoa majibu kutokana na madai kwamba baadhi ya vijana hao wamekamatwa
kwa matakwa tu ya polisi.
Alisema
kuwa anazo taarifa kuwa polisi wamejikita zaidi katika makusanyo,
badala ya kuangalia usalama wa watu na ndiyo maana wamekuwa si watu wa
kuzuia tena uhalifu kama inavyotakiwa lakini wanasubiri matukio
yafanyike.
Alitaka
polisi pia watoe sababu za kwa nini wananchi wanasema kuwa kumeibuka
kitengo cha dhuluma, ambacho wamekibatiza kuwa ‘kuingia bure na kutoka
kwa hela’, jambo linalotia doa chombo hicho.
Kwa
upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali (IGP)
Ernest Mangu, alisema jeshi hilo linakabiliwa na changamoto kubwa
ikiwemo uhaba wa vifaa na mafunzo katika kipindi hiki ambacho wizi wa
mitandao unaonekana kupamba moto.
IGP Mangu alikiri kuwepo baadhi ya polisi ambao wanatumia vibaya viapo vyao na kusababisha shutuma kwa jeshi zima.
Hivi
karibuni, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
alitangaza kuwakamata zaidi ya vijana 1,500 kuwa madai ni Panya Road.
0 comments:
Post a Comment