Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amekanusha taarifa
zilizoandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini likiwemo gazeti
la Mtanzania kuwa amempeleka Diamond polisi kwa kile kinachosemwa ni
kumtapeli shilingi milioni 10.
Martin ameiambia Bongo5 kuwa Wema na Diamond hawadaiani chochote na kwamba habari hizo ni za uongo.
“Unajua tatizo ni kwamba hatujajua source ni nani,” amesema Martin.
“Kwa sababu taarifa ikishaingia kwenye social network everybody posts,
kwahiyo sisi tunamtafuta nani ameianzisha hiyo stori. “We don’t have any
issue with Diamond. Diamond hana issue yoyote na Wema,” amesisitiza.
“Kwahiyo tunashangaa ni kama ambavyo wanazusha sijui kafumwa
na nani ni uongo mtupu. Lakini nashangaa media ambazo zinaaminika
zinaamua kuandika story bila kumpigia simu mhusika au meneja na kuuliza
ukweli wa hiyo story.”
Martin Kadinda: Wema Sepetu Hajampeleka Diamond Mahakamani Kwa Deni La Milion 10
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment