Huku kukiwa na tabia kuwa baadhi ya wanawake wanapokuwa wajawazito
wanakuwa na tabia za kusumbua na kubagua baadhi ya vitu, msanii wa
filamu za Kibongo Aunty Ezekiel ‘Mama Kijacho’, amesema kwa upande wake
yuko vile vile na wala hajabadilika.
Akiongea na mpekuzi, Aunty alisema kuwa haoni kama amebadilika
kitabia au kuwa msumbufu bali anajiona yupo kawaida ingawa mara nyingine
anakuwa anachoka sana.
“Mimba wala haijanibadili maisha kwa maana sipo kama wanawake wengine
wanavyokuwa wasumbufu, naamini kuwa nitaendelea kuwa hivi hadi mwisho
nitakapojifungua,” alisema Aunty.
Aunt Ezekiel: Mimba yangu Imekuja Vizuri Haijanibadili Tabia Kama Wengine
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment