Polisi
mkoani Klimanjaro inamshikilia mzee Mungai Molel(75) kwa tuhuma za
kumbaka mtoto wa miaka 11 wa shule ya msingi Okaseni na kumjeruhi vibaya
sehemu za siri.
Kamanda
wa Polisi mkoani humo Geofrey Kamwela, amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kwamba lilitokea Novemba 12 mwaka huu saa 12:00 jioni kijiji cha
Kitandu kata ya Uru Kusini.
Kamwela alisema mtuhumiwa huyo alimwita mtoto huyo nyumbani kwake na kumfanyia kitendo hicho cha kikatili.
“Alimwita
nyumbani kwake na kumbaka kwa nguvu na kumsababishia maumivu makali
sehemu za siri na kusababisha mtoto huyo kulazwa katika Hospitali ya
KCMC” alisema Kamwela.
Kamanda
Kamwela alisema mtoto huyo yupo katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa
matibabu kutokana na kuharibika vibaya sehemu za siri .
Alisema
mzee huyo alimbaka kwa nguvu mtoto huyo hali iliyomsababisha mtoto
kupiga makelele na kuokolewa na majirani wa mzee huyo na kutoa taarifa
polisi kutokana na kwamba walimkuta mtoto huyo akivuja damu nyingi.
Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na kwamba atafikishwa mahamani upelelezi utakapo kamilika.
Aidha
Kamanda Kamwela aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la
Polisi nchini katika kufichua matukio mbalimbali ya kihalifu ili kuweza
kunusuru maisha ya wananchi na mali zao, huku akiahidi jeshi kuendeleza
ushirikiano huo.
0 comments:
Post a Comment