MUME WA MTU NUSURA AUAWE NA KAHABA BAADA YA KUGOMA KUMPA MALIPO YAKE....!!
WAKATI Oparesheni Fichua Maovu katika jamii inayoendeshwa na Global ikiwa kazini, wikiendi iliyopita ilinasa timbwili zito la aina yake kwa mwaka 2013 ambapo mume wa mtu, Joseph Hussein (31), nusura auawe na kimada...
Hatoki mtu hapa: Joseph Hussein akiburuzana na kimada wake Neema Samson baada ya kudaiwa kupenda vya bure.
Tukio hilo lililokusanya umati lilijiri maeneo ya Mwenge, Dar mishale
ya saa 10 usiku ambapo mwanaume huyo, mkazi wa Tegeta, alikiri kupokea
kipigo almanusra apoteze uhai kutoka kwa mwanamke huyo aliyetambuliwa
kwa jina Neema Samson, mkazi wa Buguruni.
Habari za uhakika ni kwamba Neema alidai kuwa mwanaume huyo ambaye ni
mume wa mtu ana tabia ya kumtafuta yeye kwa ajili ya huduma ya mapenzi
lakini akishakidhi matakwa yake huwa hataki kutoa fedha kama
wanavyokubaliana.
Starehe gharama: Joseph akizidi kupewa hali ngumu na Neema, pembeni wananchi wakianza kusogea eneo la tukio.
SEKESEKE LAFUNGA MTAA
Kutokana na sekeseke hilo la kupigana, watu kibao walitoka nje ya
nyumba zao na kushuhudia kilichotokea ambapo walipigwa na butwaa huku
wakilalamika kuwa waliamshwa usingizini na watu waliokuwa kwenye starehe
zao.
WAAMKA NA BOKSA, NIGHTDRESS
Huku wakiwa na boksa, night dress, vipensi na wengine mataulo, majirani
wa eneo hilo walimshuhudia Neema akiwa amemkaba Joseph shingoni hadi
akashindwa kupumua na kusababisha hekaheka mtaa mzima.
“Kha! Mwanamke amemkaba mwanaume anataka kumuua kisa ni nini?” alihoji mmoja wa majirani hao.
Neema alikuwa akimnyonga Joseph kwa kutumia fulana yake akilalama kuwa amezoea kupewa penzi kisha kuingia mitini bila kulipa.
“Namjua ni mume wa mtu, ni kweli nimefanya naye mapenzi na kama
hamuamini niwaoneshe (huku akipandisha nguo na kubaki mtupu), nataka
buku kumi na tano yangu la sivyo namtoa roho,” alisikika Neema akifoka
kwa hasira.
Wakiwa eneo la tukio, mjumbe wa nyumba kumi alifika na kuwashuhudia
wakigaragazana mchangani ambapo Joseph alidai kuwa Neema alimwibia simu
yake aina ya Nokia.
MJUMBE ATEMA CHECHE
Kwa upande wake, mjumbe wa nyumba kumi alijitahidi kwa uwezo wake wote
kuwaamua lakini ilishindikana kwani Neema aliendelea kumkwida Joseph
akidai ujira wake kwani tayari simu aliyokuwa ameisunda kwenye nyeti,
alikuwa ameshanyang’anywa na wasamaria wema.
SOO HILOOO POLISI
Wawili hao waliendelea kuvutana hadi wasamaria wema waliposhirikiana
kuwabeba kisha kuwapakiza kwenye Bajaj na kuwapeleleka kituo cha
polisi....
Safari kuelekea kituo cha polisi: Wananchi wakiwabeba msobemsobe kuwapandisha kwenye Bajaj tayari kuelekea kituo cha polisi.
0 comments:
Post a Comment