Dawa ya jino bila kung’oa


Dawa ya jino bila kung’oa
Maumivu ya jino ni moja ya maumivu mabaya sana kuyapata, maumivu mengine mabaya zaidi ni maumivu ya sikio. Jino linaweza kupatwa na maumivu ambayo yanaweza kupelekea jino kutoboka na hata kuong’olewa kabisa. Dawa zifuatazo zinaweza kutuliza maumivu ya jino na hata kuliziba kabisa iwapo tayari limeanza kutoboka.

1. Asali yenye mdalasini
Chukua asali vijiko vidogo vitatu na uchanganye na mdalasini ya Unga kijiko kikubwa kimoja. Pakaa mchanganyiko huu kidogo kidogo juu ya jino linalouma kutwa mara 3

2. Aloe vera (mshubiri)
Pata aloe vera fresh na uchane kupata maji maji yake (utomvu) na unyunyize juu ya hilo jino linalouma kidogo kidogo kutwa mara 2

3. Mafuta ya nazi na karafuu
Chukua karafuu 3 zitwangwe kwenye kinu, changanya na mafuta ya asili ya nazi kijiko kidogo kimoja  uliyotengeneza mwenyewe nyumbani. Pasha kwenye moto kama dakika tatu, ipua na usubiri mchanganyiko wako upoe. Paka mchanganyiko huu juu ya jino linalouma na uache kwa dakika 7 kisha jisukutue kinywa na maji.

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger