Mtoto msichana wa miezi mitatu anaitisha chakula vizuri napohisi njaa.
– Mtoto huyo msichana kwa jina Joy Wangila anaomba chakula na kuzungumza na majirani vizuri kabisa
Wakazi wa kijiji kimoja katika eneo la Magharibi mwa Kenya wameachwa vinywa wazi baada ya mtoto mchanga kuzungumza kama mtu mzima.
Wakazi katika kijiji cha Bilaa B kwenye eneo bunge la Tongaren, Kaunti ya Bungoma, walishangaa kumsikia mtoto huyo msichana kwa jina Joy Wangila akiomba chakula na kuzungumza na majirani vizuri.
Mtoto wa miezi mitatu amewashangaza wakazi wa Bungoma kwa kuzungumza vizuri kabisa kama mtu mzima.
Ni kisa ambacho kimefanya kijiji hicho kuwa maarufu kwani kimefurika
wageni kutoka sehemu mbalimbali wanaotaka kushuhudia moja kwa moja
maajabu hayo.
Familia ilipigwa na butwaa kumsikia mtoto huyo mchanga akizungumza,
na sasa wamekuwa kivutio kijijini kwani watu wanafurika nyumbani kwao
kushuhudia maajabu hayo.
“Mwanangu anatamka maneno …akitaka chakula anaomba vizuri kabisa. Ukikataa kumpatia anaangua kilio,” Mama Salome alisema kumhusu mwanawe.
Nyanyake mtoto huyo alisema kuwa alianza kuzungumza Agosti 2, 2016.
“Mamake alitaka kumnyonyesha lakini mtoto alitaka uji.
“Nikamsikia tena akizungumza nilipokuwa nikichimbua viazi ili kuvitayarisha kwa chakula cha mchana. Jirani alikuja kuomba viazi hivyo na mtoto huyo akamuambia asithubutu kuja nyumbani hapa kula chakula chochote,” alieleza kutoka kijiji hicho cha Bilaa B mjini Bungoma.
source:http://www.muungwana.co.tz
0 comments:
Post a Comment