Wachezaji 7 waliosajiliwa mkwanja mrefu na klabu zao za zamani

 Pogba yuko mbioni kurejea kunako klabu ya Manchester United akitokea klabu ya Juventus kwa ada itakayavunja rekodi ya dunia ya paundi ml 100.

Alisajiliwa na Juventus akitokea klabu ya Manchester United mwaka 2012 baada ya kumaliza mkataba wake na klabu hiyo. Sasa amekuwa mchezaji wa kiwango cha juu ulimwenguni baada ya kutoa mchango mkubwa kwa Juve kutwaa taji la Serie A mara nne mfululizo.

Endapo dili hilo litawafanikiwa basi Pogba atakuwa ameungana na wachezaji hawa ambao awali waliondoka klabu zao na kurejeshwa kwa donge nono.

7. Marco Reus – Borussia Dortmund
 Mshambuliaji huyu alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Borussia Dortmund kabla ya kwenda timu ya vijana chini ya miaka 19 ya Rot Weiss Ahlen.

Baada ya Borussia Monchengladbach wakamsajili kutokea hapo kabla Dortmund kumrejesha tena kwa ada ya paundi mil 14.5 mwaka 2012.

6. Peter Crouch – Tottenham Hotspur

Crouch ni zao la miamba hiyo ya White Hart Lane lakini aliuzwa kwa Queens Park Rangers mwaka 2000 kwa ada ya paundi 60,000. Baadaye alirudi tena mwaka 2009 kwa ada ya paundi mil 10.

5. Nicolas Anelka – Paris Saint Germain
Nicolas Anelka alianza maisha yake ya soka akiwa na Paris Saint Germain kabla ya kuhamia Arsenal mwaka 1997 kwa ada ya paundi 500,000.

Baadaye Mfaransa huyo alihamia tena Real Madrid kabla PSG hawajamrudisha mwaka 2002 kwa ada ya paundi mil 22.

4. Mats Hummels – Bayern Munich
 Mats Hummels alikuwa ni zao la Bayern Munich kabla kuhamia Borussia Dortmund mwaka 2009 kwa ada ya paundi mil 1.

Mapema kwenye usajili wa kiangazi msimu huu, Munich waliamua kumrejesha kwa ada ya paundi mil. 28.

3. Nemanja Matic – Chelsea
Mwaka 2009, Matic alisajiliwa na Chelsea kutoka klabu ya MFK Košice kwa ada ya paundi mil 1.5 kwa mkataba wa miaka minne, lakini alihamia Benfica ya Ureno kwa ada ya paundi mil 21 huku akibadilishwa na beki Mbrazil David Luiz miaka miwili baadaye.

Akiwa Benfica alicheza vizuri na mwaka 2014 Chelsea kuamua kumrejesha kwa ada ya paundi mil 21.


2. Paul Pogba – Manchester United
 Aliondoka bure Man United wakati huo ikiwa chini ya kocha Sir Alex Ferguson mwaka 2012 na kuhamia Juventus. Ameichezea michezo zaidi 100 Juventus na sasa United wanatajwa kutaka kutoa kitita cha paundi mil 100 kumrejesha kiungo huyo, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 23.

1. Cesc Fàbregas – Barcelona
 Mhispania huyu alitokea kwenye academy ya La Masia iliyo chini ya Barcelona na kujiunga na Arsenal mwaka 2003.

Mwaka 2011, Fàbregas alirejea tena Barcelona kwa ada ya paundi mil 35 baada ya kuichezea Arsenal zaidi ya michezo 300.

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger