SERIKALI itaanzisha kitengo maalumu cha kupambana na ujangili nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema hayo juzi wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari. Alisema sasa kitengo cha kupambana na ujangili kinakwenda kuanzishwa na kitajishughulisha na uandaaji na kutoa marejeo ya wanyamapori.
Maghembe alisema kumekuwa na ujangili mkubwa wa tembo na faru ambapo takwimu zinaonesha mwaka 2009 kulikuwa na tembo 110,000 katika mbuga na mapori, lakini mwaka 2015 tembo walihesabiwa tena na walikuwa 55,000. Alisema kwenye mapori majangili wamekuwa wakitumia silaha za kivita.
“Sasa tunakabiliwa na changamoto ni namna gani tunapambana na wanaotumia silaha za kivita tunataka kudumisha utumishi wa askari hao ambao kimsingi ni raia,” alisema.
Akizungumzia kuvuna misitu na vibali alisema katika ziara ya Waziri Mkuu Julai 18, mwaka huu, alisema amezingatia pendekezo la wizara kuwa mazao ya misitu, hasa magogo na kuongeza kuwa katika kanuni za misitu hakuna ruhusa ya kusafirisha mazao ya misitu usiku, lakini watu wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea.
“Kuanzia sasa hakuna ruhusa kusafirisha mazao ya misitu usiku na wala kuisafirisha kwenye makontena inatakiwa kuwekwa kwenye magari ya wazi,” alisema na kuongeza kuwa watu wamekuwa wakikamatwa kwa kusafirishwa mazao ya misitu usiku na kupigwa faini, lakini mazao hayo yanatakiwa kutaifishwa pia.
Alisema Januari mwaka huu ukaguzi ulifanyika na watumishi wengi walisimamishwa kazi, tume imeundwa na wote watakaothibitika watachukuliwa hatua.

0 comments:
Post a Comment