Baada
ya subira ya wiki mbili ili wenyeviti na wajumbe Mtaa wa Migombani –
Segerea, Dar es Salaam waapishwe na mamlaka husika bila mafanikio,
wananchi wameamua kuwaapisha viongozi hao kwa kutumia wakili binafsi.
Wakati
hali hiyo ikitokea Dar es Salaam, wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro
baadhi ya wenyeviti wa vijiji walioshindwa wamekataa kuwaachia ofisi
viongozi wapya wakidai kuwa ofisi hizo ni mali ya CCM.
Katika tukio la Segerea lilitokea jana asubuhi Segerea Mwisho, Japhet Kembo aliapishwa kuwa ‘mwenyekiti’ pamoja na ‘wajumbe’ watatu ambao ni Rose Bernard Mhagama, Nyangeto Justin na Ramadhan Seif wote wa Chadema bila kuishirikisha Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Akizungumza
baada ya kuapishwa, Kembo alisema wananchi wamechoshwa na danadana
wanazopigwa na Manispaa ya Ilala za kutowaapisha viongozi waliowachagua.
“Wananchi wamemtafuta wakili ambaye amekuja kusimamia suala hili kisheria na ndiyo maana zoezi limefanywa hadharani,” alisema Kembo.
Kembo alisema katika nafasi ya uenyekiti alipata kura 547, Uyeka Idd wa CCM kura 273 na Erick Mchata wa NCCR-Mageuzi kura 205.
0 comments:
Post a Comment