JACKLINE WOLPER AMJIBU MBAYA WAKE ALIYE TANGAZA KUWA YEYE NI KAHABA....!!
Msanii nyota wa filamu bongo, Jacqueline Wolper amewataka wasanii wa bongo movie kuacha tabia ya kupigana majungu ya kinafiki ambayo huchangia kujenga bifu za kijinga....
Akiongea na mpekuzi wetu, wolper alidai kuwa kuna mipaka ya watu kuishi lakini kuna baadhi ya wasanii wanaamini kwamba majungu ndo mshahara wao kiasi kwamba wasipomsengenya mtu basi hawawezi kuishi...
Wolper anadai kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii wanaosemwa sana kwa mabaya hasa kuhusu maisha yake ya kila siku.Hali hiyo inatokana na umaarufu alionao ambao huwafanya wasanii wenzake wamchukie hasa wasanii wa kike...
Hii ni kauli ya Wolper alipoongea na mpekuzi:
"Wasanii tungekuwa na ushirikiano kama nisha tungefika mbali sana.
"Mimi simuogopi mtu katika maisha yangu, lakini ninachohitaji katika maisha yangu ni Heshima.
"Ukiona nimekukwaza, basi njoo nyumbani au nambie nikufuate ili tuyamalize kibinadamu na si kudhalilishana mitandaoni...
"Kuna msanii mmoja wa kike amekuwa akinichafua sana mitandaoni kwa kuniita kahaba, najiuza na matusi mengine kibao.
"Huyo ni mtu anayetafuta pakutokea, anatafuta kujulikana kupitia Wolper na pengine kafulia na sasa anatafuta mtaji.
"Tangu anitukane sikuona haja ya kumjibu kutokana na heshima niliyo nayo katika kazi yangu na heshima yangu kwa wazazi , ndugu na jamaa.
"Niliamua kumwachia mungu.Kama ni kahaba au najiuza, mungu anajua.Alisema Wolper.
0 comments:
Post a Comment