AIBU: MBUNGE AOMBA BANGI IRUHUSIWE KUWA ZAO LA BIASHARA TANZANIA , ADAI TUMBAKU INA MADHARA MENGI KULIKO BANGI...!!
Chama cha mapinduzi(CCM) kiko mbioni kujadili mpango wa kulifanya zao la Haramu la Bangi kuwa zao halali la Biashara hapa Tanzania.
Hii inafuatia mielekeo na kauli kadhaa kutoka kwa makada wake wakiwemo wabunge na Mawaziri, Kwa mfano;
1/Kauli ya jana Bungeni kutoka kwa Naibu waziri wa Kilimo na chakula Adamu Malima kusema ITALIFANYIA KAZI WAZO LILITOLEWA BUNGENI NA MBUNGE WA CCM KUTAKA BANGI IHALALISHWE KULIMWA KIBIASHARA!!
2/Ushauri wa Mbunge wa CCM, Ally Keisy Mohammed jana bungeni ...
-Akiuliza swali la nyongeza, Mbunge wa CCM Ali Keisy
Mohamed amesema tumbaku ina madhara mengi lakini serikali bado
inalitambua kama zao la biashara, ameuliza kwa nini serikali sasa
isipeleke nguvu kwenye bangi kwani kuna sehemu inaruhusiwa.
3/Kauli za Mbunge wa CCM, Mohamed Lugora kuwa ana list ya mawaziri kadhaa wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya(Bangi ikiwemo) aliyoitoa jana Bungeni.
4/Kauli ya mbunge wa Tarime kwa tiketi ya CCM, Nyambari Nyangwine ya kutaka Bangi ihalalishwe kibiashara huko Tarime jimboni mwake.
5/Kauli ya Naibu Spika wa bunge Job Ndugai(CCM) kuwa wabunge wengi ni wavutaji wa Bangi wazuri sana.
6/Makada wakubwa kadhaa wa CCM waliwahi kukamatwa na polisi na shehena kubwa sana ya bangi wakiuza na kusafirisha.
7/Habari za kuwepo mashamba makubwa mengi sana hapa Tanzania ya Kilimo cha Bangi yakimilikiwa au kufadhiliwa na makada wakubwa CCM.
0 comments:
Post a Comment