SHEHENA KUBWA YA SUKARI ILIYOIBIWA NA MAJAMBAZI HAPA BONGO YAKAMATWA...
Shehena
ya sukari yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tisini iliyoibiwa
na majambazi kwa kutumia silaha na kuwakata mapanga kichwani baadhi ya
walinzi katika moja ya ghala ya kuhifadhia bidhaa eneo la Mbagala rangi
tatu jijini Dar es salaam zimekamatwa na jeshi la polisi huko Chamazi
kabla ya kufikishwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa.
Baada
ya kupatikana kwa fununu ya kukamatwa kwa shehena ya mifuko mingi ya
sukari, ITV ilitua katika ofisi za polisi wilaya ya Mbagala maarufu kwa
jina la kituo cha Maturubahi ili kujionea ukweli, ambapo camera ya ITV
ilishuhudia lori kubwa yenye namba za usajili T.524 AJZ aina ya scania
ikiwa imepakia mifuko ya sukari ambazo tayari zilikuwa zimeibiwa usiku
wa tarehe 4 mwezi August 2013.
Baada
ya ITV kushuhudia mifuko 1312 za sukari, ambayo kila mfuko ina kilo
hamsini, ITV ililazimika kufika eneo la Mbagala rangi tatu katika ghala
ya bwana Haruni Zakaria mmiliki wa kampuni ya Al-Naiem Enterprises
ambapo sukari hiyo ilihifadhiwa na kukuta damu katika maeneo ambayo
walinzi wa ghala hiyo walipigwa na kufungwa kamba kama anavyoeleza
kamanda wa mkoa wa Temeke ACP Englibert Kiondo.
Wakati
tukio hilo linatokea baadhi ya majambazi hao walijitahidi kufanya kila
waliwezalo ili kuzimisha sakata hilo,lakini maafisa wa jeshi la polisi
waliamua kusimamia maadili yao ya kazi kwa kukataa rushwa huku
wakiwabana wahusika hao kijeshi ili kutaja mtandao mzima wanaohusika
ambapo maafisa wa jeshi walifanikiwa kufika hadi Chamazi eneo
linalotumika katika kuficha sukari kabla ya kusambaza sokoni.
Kutokana
na tukio hilo kuleta hisia kwa wakazi wa maeneo hayo,licha ya
watuhumiwa kumi na mbili kushikiliwa na jeshi la polisi, lakini baadhi
ya mashuhuda walilazimika kutoa maoni yao.
0 comments:
Post a Comment