ROMA ATOA ONYO KWA VYAMA VYA UPINZANI TANZANIA


Zikiwa zimebaki takribani wiki nane kufikia siku ya uchaguzi mkuu wa raisi, wabunge na Madiwani nchini Tanzania, Rapper mahiri katika Game ya Bongo flava Roma Mkatoliki, amevishukia vyama vya Upinzani vinavyotumia ngoma zake za Pastor na Tanzania katika kampeni zao za kisiasa bila ruhusa kutoka Roma amesema amewahi kushuhudia moja wapo ya Kampeni ya kisiasa ikitumia nyimbo zake, Roma amevionya vyama hivyo kuacha mara moja, au wamfuate kuongea nae ili waelewane kibiashara.

255 ilipotaka kujua kuhusu ni chama gani cha siasa yupo tayari kufanya nacho kazi…….Roma akajibu kuwa yupo tayari kufanya kazi na chama ambacho kitakua kinaenda sawa na misingi ya misimamo yake aliyokwisha kuitoa katika nyimbo zake za Tanzania na Pastor(chama chenye sera na nia ya kuboresha maisha ya Watanzania ndio chama ambacho huenda Roma atakiunga mkono)

Aidha Roma amesema ametoa muda kwa Vyama vya siasa vya Upinzani vinavyotumia ngoma zake katika mikutano yao na kampeni kumfuta ama kuacha kutumia, la sivyo atachukua hatua kali za kisheria dhidi ya wahusika hao, kwani wao wananufaika kwa kuwavuta mashabiki kwa kivuli cha nyimbo zake.

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger